MY LIFE MY CLOTHES...

January 17, 2018 Being Anastazia 0 Comments

Whats culture and whats tradition?and who are you to decide for me?

Kwanza hizi lugha za watu hamtanielewa, nimesikitishwa na uamuzi wa serikali ya mkoa wa dar es salaam kukamata wanaovaa nguo “fupi” “milegezo’’ na “viduku”. Nimejiuliza sana wametumia vigezo gani katika kufanya maamuzi haya? Sababu kwangu naona yamekaa kisiasa, kidini na kimtazamo zaidi yaani aliye na madaraka akiona kwake kiduku kinamchefua basi atasema si utamaduni wa mtanzania, nguo fupi haipendi atasema si utamaduni wa mtanzania!! Hii ni Too Much..
Tuzungumzie kidogo kuhusu sababu zilizotolewa kuhusu ukamataji wa wanaovaa nguo fupi na kunyoa viduku?
MAADILI?
Maadili kwa mujibu wa nani? Utamaduni gani tunaongelea hapa?
Maana ninavyofahamu tanzania tuna makabila zaidi ya 120 na kila kabila linautamaduni wake na mtazamo wake kimaadili. Au yameandikwa katika katiba ambayo inaitwa ya kidemokrasia?
UTAMADUNI?
Tunawajua wazaramo ambao ndio wakazi haswaa wa dar es salaam, unajua utamaduni wao? Unakataza nguo fupi? Unakataza kunyoa kiduku au rasta?
Tuelezane vizuri jamani pengine sisi hatujui kuhusu hivi vitu..
NINACHOONA MIMI
Mi naona tu siasa na maono ya imani za watu kidini ndio zinazolazimisha haya mambo ingawa najua serikali yangu haina dini na ni ya kidemokrasia hivyo kila mtu an haki ya kuwa vile anvyotaka.
MORE OVER
Dar es salaam ni moja ya miji yenye joto duniani ambapo sitarajii watu kuvaa suruali na mashati marefu kwa mtazamo wa kawaida. Kiafya na kistaarabu tu, ndio maana tukiingia kwenye daladala tunapata tabu kwa harufu za majasho ya makwapa yaliyonyimwa hewa ya kutosha kwa kigezo cha utamaduni. Tafadhali usinilazimishe nivae nguo kama fuko la viazi sababu tu unaamini bukta, min skirt au blauzi yangu haikupendezi sababu wote tuna haki sawa na si lazima uridhike na mavazi yangu.

Ironheart

#mylifemyclothes #nguozangumaishayangu #dontchangeme


Article by Ayubu Mbarazi.

0 comments: